Ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa KPI.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa leo ametembelea kiwanda cha dawa KPI kinachosimamiwa na MSD ,ambapo ameahidi kuwa serikali italifanyia kazi suala la kuimarisha mitambo ya kuzalishia dawa ya KPI,ambapo pamoja na mambo mengine amesisitiza watendaji wa taasisi ya KPI kuzingatia taratibu ,miongozo na sheria za kutekeleza majukumu yao,hasa upande wa manunuzi.