Sisi ni Nani
Kiwanda cha Dawa Keko (1997) Ltd) kilianzishwa mwaka 1968 ikiwa ni Idara Maalumu katika Wizara ya Afya kwa lengo la kusambaza dawa katika Bohari kuu ya Dawa nchini ambayo sasa inajulikana kama Bohari ya Dawa (MSD). Kiwanda kilijengwa chini ya usaidizi wa Serikali ya Uchina yenye uwezo wa kuzalisha dawa na vifaa vya matibabu. Kiwanda kilisajiliwa mwaka 1992 chini ya umiliki wa Serikali. Kwa mujibu wa Sheria ya Makampuni ya mwaka 2002, mwaka 1997 kiwanda kilibinafsishwa ambapo Kampuni binafsi, Diocare ilinunua asilimia 60 ya hisa na Serikali kubakiza 40% ya hisa na jina likabadilishwa na kuwa Keko Pharmaceutical Industries (1997) Ltd (KPI).
Hata hivyo, Mkataba mpya wa Wanahisa uliotiwa saini Desemba, 2019, ulihitimishwa kuwa Kampuni ya Diocare itahamisha hisa zake 30% kwa Msajili wa Hazina na sasa Serikali inamiliki hisa 70% huku Kampuni ya Diocare ikisalia na 30% ya hisa za KPI.
Kulingana na makubaliano ya wenye hisa, kama sehemu ya Ubia (JV) yenye hisa nyingi hulazimisha Usimamizi wa Kampuni. Kwa hiyo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina imechukua usimamizi wa Kampuni ya Keko Pharmaceutical Industries (1997) Ltd tangu tarehe 19 Oktoba 2020 kwa kuteua Menejimenti ya Muda ya kusimamia masuala yote ya Kampuni.
Usimamizi wa KPI uko chini ya Bodi ya Wakurugenzi ambayo ndiyo chombo cha juu zaidi cha kufanya maamuzi ambacho kinasimamia na kuweka mwelekeo wa KPI. Mwenyekiti wa Bodi anateuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wajumbe wanne (4) wa Bodi huteuliwa na Msajili wa Hazina na wajumbe wawili (2) waliobaki wa Bodi huteuliwa na Kampuni ya Diocare. Shughuli za kila siku za kampuni ni jukumu la timu ya Usimamizi inayoongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu. KPI ni kampuni inayojihusisha na biashara, ambayo imedhamiriwa kujiendesha yenyewe bila kutegemea ruzuku za Serikali.
Kwa mujibu wa muundo wa shirika, KPI inaundwa na Kurugenzi tatu (3), Vitengo nne (4) na Idara nne (4). Afisa Mtendaji Mkuu atakuwa ndiye mwangalizi wa kazi na majukumu yanayotekelezwa katika idara na vitengo vyote katika kampuni.
Maono
Kuzalisha na kusambaza bidhaa za dawa salama, zenye ubora na nafuu kwa wateja ili kulinda na kuboresha afya ya binadamu.
Dhamira
Kuwa mtengenezaji wa dawa anayeongoza kwa ubunifu barani Afrika.
Maadili
Kuwa mfano wa kutegemewa
Ubunifu
Kufanya kazi kwa kushirikiana
Uadilifu
Umakini kwa Wateja
Kuzalisha dawa zenye Ubora