Uthibiti Ubora
Idara ya Uhakikisho wa Ubora ina jukumu la kuhakikisha kuwa dawa inayotengenezwa itatoa athari inayotarajiwa kwa mgonjwa. Uhakikisho wa ubora pia unahakikisha kuwa hakuna uchafu uliopo na kwamba dawa itakidhi mahitaji ya ubora na kanuni zote husika.
Zifuatazo ni taratibu za Uhakiki wa Ubora wa dawa:
a) Ukaguzi na uhifadhi wa viambato vinavyoingia vya dawa (API), Viungwaji na Nyenzo za Ufungaji.
b) Mchakato wa utengenezaji na udhibiti wa mchakato
c) Uhakiki wa rekodi za uzalishaji
d) Kutolewa kwa mwisho au kukataliwa kwa kila kundi la bidhaa za dawa kwa usambazaji na uuzaji
Utimizwaji wa majukumu hayo hapo juu utampatia mwananchi bidhaa bora kwa afya yake kama motto wa KPI unavyosema