DIODOL®
Vidonge vya Diodol ni vyeupe vya mviringo vyenye mstari upande mmoja na maandishi KPI/GOT na 500 na upande mwingine una maandishi ya DIODOL.

Kila kidonge cha Diodol kina paracetamol BP sawa na Paracetamol 500mg.
Paracetamol hupunguza maumivu makali na ya kawaida ya kichwa na viungo pia hutuliza maumivu yanayosababishwa na magonjwa kama baridi yabisi, hedhi, maumivu ya misuli, maumivu ya meno. Pia Diodol hutumiwa kushusha homa kali.